Pages

Wednesday, July 31, 2013

WAHITIMU WALIOHITIMU ELIMU YA VYUO VYA JUU WAJIAJIRI KUPITIA KILIMO WILAYANI IGUNGA MKOANI TABORA


Viongozi wa wanakikundi cha wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu wilayani Igunga Mkoani Tabora - GIYA wakiwa katika harakati za kuandaa baadhi ya mazao ya alizeti waliyolima msimu huu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Boniphace Maganga anayefuatia ni Mweka hazina Mathiasi Ndaje,  Msanii wa sauti Oscar Nyerere ambaye aliwatembelea kijiji hapo, na Katibu wa kikundi hicho Bw. Edward Tungu.
 
 Baadhi ya alizeti ambazo zimevunwa na zipo tayari kuchambuliwa tayari kwa kukamua mafuta. Wahitimu hao wameiomba Serikali iwasaidie mashine ya kukamulia mafuta ili waweze kukamua mafuta moja kwa moja badala ya kuuza kwa makampuni yanayotengeneza mafuta.
 
 Mwenyekiti wa kikundi cha GIYA Bw. Boniphace Maganga, akionyesha moja ya sega la alizeti ambayo wameilima shambani kwao katika kijiji cha Magogo Isakamaliwa Mkoani Tabora Wilayani Igunga.
 
  Wa kwanza (kushoto) Katibu wa GIYA akiwa na Msanii Oscar Nyerere, Mwenyekiti wa kikundi  Bw. Boniphace Maganga na Mweka Hazina wa kikundi Bw. Mathias Ndaje Shambani kwao Isakamaliwa.
 
 Mto huu Manoga ambao haukauki ni hazina kubwa ya vijana hao katika kumwagilia mazao yao.
 

Mahema ambayo wanatumia kulala wanakikundi hao. Mahema hayo wamesema  yametolewa na Mkuu wa Mkoa huo Bi Fatuma Mwasa kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Elibaliki Kingu.
 
 Mmoja wa wanakikundi cha GIYA Bi Chausiku Joseph akiwa nje ya hema baada ya kazi ngumu ya shambani.
 
 
 Viongozi wa GIYA wakionesha mashine mbovu ambayo haitumiki na inahitaji matengenezo.
 
 Hili ni shamba la vitunguu ambalo limelimwa na vijana hawa lenye ukubwa wa hekari nane.
 
"Hii ndio sehemu tunayolala sisi wasomi....."  Katibu  wa kundi hilo Bw. Edward Tungi akimwelezea Msanii Oscar Nyerere kushoto (PICHA ZOTE NA IPSHA BLOG).


KUNDI LA VIJANA AMBAO NI WAHITIMU WA ELIMU YA VYUO VYA JUU-GIYA WANAOJISHUGHULISHA NA KILIMO CHA MAZAO YA BIASHARA KATIKA KIJIJI CHA ISAKAMALIWA KILICHOPO UMBALI WA KM 54 KUTOKA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA IGUNGA MKOANI TABORA, BADO WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO UBOVU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA MPAKA KUFIKA KIJIJINI HAPO JAMBO AMBALO WAMEIOMBA SERIKALI KULIFANYIA KAZI ILI KUWAWEZESHA KUTIMIZA MALENGO YAO.

WAHITIMU HAO WAKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WETU KIJIJINI HAPO WAMEELEZEA KUWA LENGO LA KWENDA KUISHI KIJIJINI HAPO NA KUINGIA KATIKA SEKTA YA KILIMO NI PAMOJA NA KUKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA HUSUSANI KWA VIJANA WANAOMALIZA ELIMU YA JUU AMBAPO PAMOJA NA MAFANIKIO WANAYOENDELEA KUYAPATA BADO WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA PEMBEJEO ZA UHAKIKA IKIWEMO MASHINE YA KUKAMULIA MAFUTA YA ALIZETI AMBAYO WANAAMINI ITAWASAIDIA KUTOKANA NA KUVUNA KIASI KIKUBWA CHA ZAO HILO KIJIJINI HAPO.

MBUNGE WA JIMBO HILO MHE. DAKTA DALALI PETER KAFUMU NA MKUU WA WILAYA HIYO BW. ELIBARIKI KINGU WAKIJIBU BAADHI YA CHANGAMOTO HIZO WAMESEMA KUWA SERIKALI IMEJIPANGA KATIKA KUHAKIKISHA KUWA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI VIJANA HAO ZINAFANYIWA KAZI KWA KUPITIA VYANZO MBALIMBALI VYA FEDHA UKIWEMO MFUKO WA JIMBO WA WAJASIRIAMALI AMBAO UMEANZISHWA NA MBUNGE HUYO KUFUTIA MSAADA WA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 10 AMBAO UMETOLEWA NA MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA IPP BW. REGINALD MENGI NA KUFAFANULIWA KUWA MFUKO HUO KARIBU UTAANZA KUFANYA KAZI KATIKA JITIHADA ZA KUSAIDIA MAENDELEO JIMBONI HAPO.    

No comments: