Pages

Sunday, April 14, 2013

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA SHILINGI MILIONI 51 KIJIJI CHA MAKANYA

 
Mhandisi wa Kampuni ya Dr Gogo engineering limited, Godwin Kalaghe (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo nyaraka za taarifa za kukamilika kwa ujenzi wa kisima cha maji katika Kijiji cha Makanya, wilayani Same juzi. Ujenzi wa kisima hicho uliogharimu sh. mil. 51.6 ulifadhiliwa na TBL.
Mradi wa kisima cha maji ambao umefadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania TBL katika kijiji cha Makanya wilayani Same. Mradi huo una thamani ya shilingi milioni 51.6. Uwepo wa kisima hicho utasaidia kupungua kwa tatizo la maji kwa wakazi wa Tambarare katika wilaya ya Same.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Makanya, wilayani Same, Asia Zuberi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji kwa msaada wa TBL kwa gharama ya Sh. mil. 51.6.  Hafla hiyo ilifanyika kijijini hapo juzi.
 

No comments: