Pages

Friday, April 12, 2013

RAIS ATEUA MKURUGENZI MKUU - NEMC


Mhandisi Bonaventure Baya


RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amemteua kwa mara ya pili Mhandisi Bonaventure Baya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC ) kwa kipindi kingine cha miaka mitano (5).

Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Tutubi Mangazeni, Baya pamoja na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC pia ni Rais wa kwanza wa Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Wataalamu wa Mazingira Nchini.

Bwana Baya pia ameshawahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Huduma ya Misitu na Mjumbe wa Bodi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

1 comment:

Anonymous said...

Heya! I'm at work browsing your blog from my new apple iphone! Just wanted to say I love reading your blog and look forward to all your posts! Keep up the superb work!

Feel free to surf to my weblog - hotel opole