
Kazi ya
uokoaji wa watu ambao wamefukiwa na mgodi uliokuwa unatumika kuchimba kokoto imekamilika ambapo miili ya watu 14 imepatika.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa huo Magese Mwilongo zinasema kuwa hali za watu wawili ambao wameokolewa katika mgodi huo bado ni mbaya na wamelazwa katika hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.
Kufuatia ajali
hiyo mgodi huo umefungwa kuendelea na shughuli zake ambapo kumbukumbu
zinaonyesha kuwa hiyo sio mara ya kwanza ajali kama hiyo kutokea katika mgodi
huo. Miaka saba iliyopita ajali nyingine ilitokea na kusababisha vifo vya watu saba.
Tukio hili linatokea ikiwa ni siku tatu baada ya maafa mengine kutokea jijini Dar es Salaam ambapo watu takriban 30 wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa 16 kuanguka.
No comments:
Post a Comment