Mbunge wa Chambani-Pemba, Kisiwani Zanzibar Salim Hemed Khamis ambaye jana aliugua ghafla wakati wa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ofisi ndogo jijini Dar es Salaam amefariki.
Khamis, mara baada ya kuugua ghafla alisaidiwa na Wabunge wenzake na Maofisa wa Bunge na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa matibabu na mchana huu amefariki dunia.
Taratibu za kuusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.
Kwa hisani ya Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment