Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Dkt. Dorothy Gwajima akifungua kikao cha Kamati ya ushauri na uratibu wa
utekelezaji wa ahadi za nchi katika jukwaa la kizazi chenye usawa,
kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 11/05/2022.
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake
na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Katibu Mkuu Dkt. Zainab
Chaula pamoja na wajumbe wa Kamati ya ushauri na uratibu wa utekelezaji
wa ahadi za nchi katika Jukwaa la kizazi chenye usawa baada ya ufunguzi
wa kikao cha Kamati hiyo kupokea na kujadili mpango kazi wa utekelezaji
wa ahadi hizo kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 11 Mei, 202
Na WMJJWM, Dodoma
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy
Gwajima amewataka Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa kukamilisha Maazimio ya
Beijing ya miaka 27, tangu Beijing iweke maazimio ya kuwa na kizazi
chenye Usawa kwani ndio matamanio ya Mhe. Rais Samia.
Aidha
amewata Wajumbe wa Kamati hiyo ya Kitaifa ya kushauri na kuratibu
utekelezaji wa ahadi za nchi katika jukwaa la kizazi chenye usawa
kufanya kazi kwa weledi na kuwa chachu ya mabadiliko kuelekea kizazi
chenye usawa.
Dkt.
Gwajima ametoa rai hiyo wakati akifungua kikao cha Kamati hiyo chenye
lenyo la kupokea rasimu ya mpango kazi wa utekelezaji wa ahadi hizo,
kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 11/05/2022.
Mhe.
Dkt. Gwajima amesema Kamati ikifanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha
ahadi za nchi zinatekelezwa katika Jukwaa, utakuwa ni mwanzo wa kizazi
chenye usawa na kuwa nchi ya mfano wa kuigwa.
"Mhe.
Rais amedhamiria kuhakikisha nchi inakwenda sambamba na ulimwengu na
haimwachi mtu nyuma kwa visingizio vyovyote hasa wanawake walioachwa
nyuma kwa miaka mingi ambako kumesababisha maendeleo duni kwa watoto wa
kiume na wa kike, hivyo tunapaswa kuhakikisha mlolongo huo tunaumaliza
ili jamii yote tuwe na kizazi cheye usawa na kuongeza kasi ya maendeleo
maradufu" alisisitiza Mhe. Gwajima.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula akizungumza katika kikao
hicho amebainisha kwamba, Kamati hiyo tangu iteuliwe imekuwa na
ushirikiano mkubwa na Wizara katika kuhakikisha matarajio ya nchi
yanafikiwa.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Angellah Kairuki ameishukuru Wizara kwa
ushirikiano katika kufanikisha kuwa na rasimu ya mpango kazi
utakaotumiwa na Kamati hiyo kufanya kazi yake ya kuratibu ahadi za nchi
kufikia kizazi chenye usawa.
"Malengo
yetu ni kuwa na mpango mkakati unaokidhi mazingira ya nchi yetu na
usiomwacha mtu nyuma, tangu Desemba mwaka jana Kamati imeshafanya vikao
vinne kwa ajili ya kupitia rasimu ya mpango kazi huu na sasa tupo tayari
kupokea" alisema Kairuki.
Kairuki ameongeza kuwa hatua zinazofuata ni kuwa na vikao kwa upande wa bara na Zanzibarambapo
Kamati itakutana na wadau wa mbalimbali kutoka Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali, sekta binafsi, vingozi wa Dini, Makundi maalum, Wasanii,
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, TUCTA, Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Zanzibar, ZATUC, Vijana na na vituo vya ubunifu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliiteua
Kamati hiyo ya Kitaifa mnamo tarehe 16 Desemba, 2021 kwa lengo la
kushauri na kuratibu utekelezaji wa ahadi za nchi katika Jukwaa la
kizazi chenye usawa, ambapo Mhe.Rais alichagua kutekeleza eneo la pili
la kuhakikisha usawa wa jinsia.
Mpango
kazi huo unaoandaliwa kwa kushirikisha wadau wa sekta zote unatarajiwa
kukamilika mwezi Juni mwaka huu ili Kamati hiyo ianze kuufanyia kazi.