TANGAZA NASI KATIKA BLOG HII. Kwa Mawasiliano: 0713/0767/0787-270376, shabanitolle73@gmail.com & ipmwaipaja@yahoo.com
Pages
▼
Thursday, June 9, 2016
MTI WA MWEMBE WAFANANISHWA NA SURA YA BABA WA TAIFA, MWALIMU NYERERE

Juzi usiku katika maeneo ya Tangamano mkoani Tanga kulizuka kizaazaa baada ya mti mmoja wa mwembe kufananishwa na taswira ya sura ya baba wa taifa, marehemu Julius Kambarage Nyerere.
Tukio hilo lilisababisha watu kujazana tangia usiku hadi asubuhi ya jana ambapo watu walikuwa wakiushangaa mti huo huku kila mtu akisema lake.
Watu hao wanadai mti huo huonesha vizuri taswira hiyo ikifika mida ya usiku na kwamba wanashangaa pamoja na mti huo kuwepo hapo miaka mingi, ni siku hiyo ndio walipoona taswira hiyo.
Wapo walioamini kuwa marehemu Baba wa Taifa ameamua kujitokeza kwa jinsi hiyo sababu ya matukio ya mauaji ya kinyama yanayotokea mkoani humo ambapo siku za karibuni watu wanane wamechinjwa na watu wasiojulikana katika maeneo ya jirani na mapango ya Amboni ya mkoani humo.

Wednesday, June 8, 2016
MWANAMKE AMWAGIWA TINDIKALI NA MMEWE; AHITAJI MSAADA WA MATIBABU
Specioza, baada ya kumwagiwa tindikali. |
Na. Ipyana A. Mwaipaja
Mwanamke mmoja mkazi wa Mwanza, Speciosa Sylvester amefanyiwa ukatili wa kumwagiwa tindikali mwilini na anayedaiwa kuwa mume wake.
Akielezea kisa kizima jana kupitia kipindi cha Leo Tena cha redio ya Clouds FM kinachorushwa kuanzia saa 4 hadi 7 mchana, Bi Speciosa amesema siku ambayo alimwagiwa tindikali alikuwa Mwanza ambapo alihamisha makazi yake kutoka Kahama baada ya kushindwa kuishi na mumewe ambaye alikuwa akimnyanyasa na kumtesa sana.
“Niliamua kuachana nae na kuondoka na kumuachia mali zote tulizochuma wote ambazo ni shule iitwayo Jerusalem English Medium, magari 8 na nyumba 3. Alikuwa anatembea na walimu ovyo na pia alifukuza wanangu alionikuta nao, hivyo nikawa sina budi bali kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya Mwanza," amesema Speciosa.

Speciosa amesema kuwa wakati anaoana na mume huyo alikuwa tayari ana watoto wawili wa mume wa kwanza aliyefariki na alifanikiwa kuzaa watoto wengine wawili na mume huyo mpya kwa kipindi cha miaka 10 ambayo ameishi naye.
Speciosa amesema baada ya yeye kuondoka huku nyuma mumewe shule ilimshinda kuiendeleza, wanafunzi wakapungua hivyo akawa hana jinsi ikabidi amtafute yeye ili arudi kumsaidia.
Mume huyo alimtafuta na kufanikiwa kumpata huko Mwanza alipokuwa anaishi na wakati huo akiwa na 'grocery' yake. Alipompata alimbembeleza sana arudi lakini yeye alikataa kabisa sababu hakutaka kurudi tena kwenye mateso.
“Siku moja alikuja nilipokuwa nafanya kazi nikamkaribisha na baadaye akataka kwenda kuwaona wanae nikampeleka akawaona. Kesho yake akaja tena na kuendelea kunibembeleza nirudi Shinyanga lakini nilimkatalia kabisa na kumwambia kuwa yeye aendelee na maisha yake kwani mimi nimeshasamehe kila kitu nimeanza maisha upya,” amesema Speciosa.
Mwanaume huyo hakukata tamaa kwani aliendelea kuwa anakuja Mwanza kumbembeleza na kurudi Shinyanga kwa muda wa kama miezi miwili bila mafanikio na ndipo siku moja alipokuja, wakati anaongozana nae kurudi nyumbani alitokeza kijana na kummwagia kitu machoni na mwilini ambacho baadaye iligundulika kuwa ilikuwa ni tindikali.
"Siku ya tukio alikuja tena grocery kwangu akanikuta naumwa nikamwambia nataka kufunga mapema sababu sijisikii vizuri. Baada ya kufunga wakati naondoka akawa anaongozana na mimi akiniambia niende nae mahali akaninunulie kuku nile lakini nilikataa. Akaniambia kwa mara ya mwisho umeamua kujivua gamba? umeamua hurudi tena kwangu? ndipo ghafla akatokea huyo kijana na kunimwagia tindikali. Nikawa namuita akawa haniitikii kisha baada ya dakika kama kumi alirudi huku akisema wana mapanga kisha na yeye akakimbia," amesema Speciosa.
"Nilirudi nyumbani kuwapa taarifa wanangu kuwa nimemwagiwa tindikali na niliwaambia wanangu kuwa sio baba yao aliyenimwagia tindikali sababu wanajua mgogoro uliopo kati yangu na baba yao. Nilipata matibabu hospitali ambapo nilitolewa nyama ya kwenye paja na nilipotoka hospital mume wangu alinichukua na kunirudisha nyumbani kwake kahama," amesema.

Akiendelea kuelezea kwa uchungu, Speciosa amesema baadae alitakiwa aende hospitali ya Muhimbili iliyopo Dar es Salaam ili kufanyiwa upasuaji na mumewe huyo aliongozana nae hadi Dar es Salaam ili ampeleke hospitalini hapo. Gharama zote za matibabu yake tangu siku ya tukio zilikuwa zikilipwa na mumewe huyo. Wakiwa katika nyumba ya wageni jijini Dar es Salaam, siku ambayo ndio alitakiwa kufanyiwa upasuaji, ndipo mumewe huyo alipoamua kuvunja ukimya na kumwambia kuwa ni yeye ndiye aliyemfanyia tukio hilo.
"Tulikuwa gesti akaniuliza kwamba nikimjua aliyenimwagia tindikali nitafanyeje? Mimi nikamwambia sitamfanya chochote, nimeshamsamehe. Ndipo akaniambia kuwa ni yeye ndiye aliyenimwagia tindikali na amenimwagia kwa kuwa nilikuwa nakataa kurudi kwake......Nililia sana mpaka nikashindwa kufanyiwa oparesheni siku hiyo kwa kuwa presha ilipanda. Mpaka hapo sikuwa nimegundua kuwa mume wangu ndiye aliyenifanyia ukatili huo kwani alikuwa akijifanya yupo pamoja na mimi muda wote na kulipa gharama zote za matibabu na usafiri," amesema Speciosa.
Speciosa amesema kuwa aliogopa kumwambia daktari suala hilo na baadaye akafanyiwa upasuaji na kufanikiwa kurudi nyumbani kwa mumewe, Kahama.
Amesema tangu hapo mume wake akawa anamtishia kumuua iwapo atamwambia mtu yeyote au kushitaki Polisi kuwa yeye ndiye aliyemfanyia ukatili huo na kutokana na hilo hakushitaki popote. Siku moja akaamua kutoroka ambapo alipanda magari makubwa ya mizigo na akiwa njiani alikutana na mama mmoja ambaye aliamua kumsaidia baada ya kumweleza tatizo lililomkuta.
"Nilikutana na mama mmoja akanisaidia akaniunganisha na mama mwingine mwalimu ndio mpaka leo nipo nakaa kwake lakini bado sijapata matibabu mengine ambapo natakiwa kufanyiwa operation ya mdomo na mkono kwani nyama za mkononi na kifuani zimeshikana. Niliposikia Clouds mmemsaidia yule dada asiyeona nikaona na mimi nije mnisaidie ili watanzania wenzangu watakaoguswa waweze kunichangia nipate milioni 6 ambazo zinatakiwa kwa ajili ya upasuaji katika hospitali ya Sanitas," amesema Speciosa.
Mbali na msaada huo wa pesa ya matibabu, Specioza pia ameomba apatiwe msaada wa kisheria na yeyote atakayeguswa na tatizo lake.
Namba ya simu ya Speciosa ni 0713-535549. KUTOA NI MOYA SIO UTAJIRI, TUMSAIDIE MTANZANIA MWENZETU.

Chanzo: Clouds FM redio na Geah Habibu website.
WILL SMITH NA LENNOX LEWIS WATEULIWA KUBEBA JENEZA LA MUHAMMED ALI
Msanii mashuhuri wa filamu nchini Marekani, Will Smith na aliyekuwa bingwa wa dunia wa uzani wa juu Lennox Lewis, wameteuliwa kuwa miongoni mwa watu watakaobeba jeneza la bondia bingwa mara tatu duniani, marehemu Muhammed Ali.
Mwaka wa 2001 Smith aliigiza katika filamu kumhusu Muhammad Ali kama Ali, jambo lililosababisha kuteuliwa katika tuzo la Oscar.
Tangu hapo amekuwa rafiki wa familia hiyo ya Muhammad Ali.

Marehemu Muhammad Ali (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na muigizaji filamu maarufu Will Smith (Fresh Prince). |
Lewis kwa upande wake ni miongoni mwa mabondia watatu kwa pamoja na Ali na Evander Holyfeild ambao wamewahishinda taji la uzani wa juu mara tatu.
Wawili hao sasa wataungana na jamaa na marafiki wa marehemu Muhammad Ali kubeba jeneza lake, mjini Kentucky siku ya Ijumaa wakati wa mazishi yake.

Marehemu Muhammad Ali (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na bondia Lennox Lewis. |
Mohammed Ali alifariki siku ya Ijumaa mjini Arizona alikokuwa amelazwa hospitalini akiwa na umri wa miaka 74.
RAIS MAGUFULI AMTEUA JAJI FERDINAND WAMBALI KUWA JAJI KIONGOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 07 Juni, 2016 amemteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi.
Jaji Wambali anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaaban Ally Lila aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mkoani Tanga.
Uteuzi huo umeanza mara moja.